WELCOME TO MUSTAFA DIGITAL WORLD ACADEMY >>>>>>>> MUDWA IS YOUR SOLUTION FOR .....(HESLB APPLICATION, BIRTH &DEATH SERVICES- eRITA, UNI APPLICATIONS!, PASSPORT,TIN NUMBER etc. FOR ANY INQUIRY CALL US THROUGH>>>>>> +255719891310
Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Wednesday, 28 May 2025

MAOMBI YA MKOPO WA ELIMU YA JUU

HESLB na NIDA Kushirikiana Kuwatambua Waombaji Mikopo Kupitia NIN

Akiongea kwenye kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia, ameweka wazi kuwa namba ya utambulisho wa taifa itakuwa ni ya lazima katika kuomba mkopo kwa mwaka ujao wa masomo. “Tunatarajia kufungua dirisha la maombi ya mkopo mwezi Juni, 2025… kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 … namba ya utambulisho wa taifa itakuwa hitaji la lazima katika kujaza fomu za maombi ya mkopo, hivyo waombaji wote wanapaswa kuwa na namba hii wakati wa kujaza maombi yao ya mkopo”, amesema Dkt. Kiwia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. James Kaji, amesema kuwa NIDA wapo tayari kuwahudumia wanafunzi wote wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu na kuomba mikopo kutoka HESLB kwa kuwapatia namba za utambulisho kwa wakati na hivyo wanafunzi wanapaswa kufika kwenye ofisi za NIDA mapema ili kupatiwa namba za utambulisho. “NIDA ni maisha, kwa sasa … NIDA inaendelea kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha mifumo yote ya serikali inasomana… tunawasisitiza waombaji wote wa mikopo ya elimu ya juu kuhakikisha wanafika mapema NIDA ili kupata namba ya utambulisho wa taifa”, ameeleza Bw. Kaji.

Monday, 28 April 2025

VITU VYA KUZINGATIA KWA MAOMBI MAPYA YA CHETI CHA KUZALIWA

Ni muhimu kwa watanzania wote wenye uhitaji wa

  1.   Kuomba cheti kipya cha kuzaliwa   
  2. Uhakiki wa cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya maombi ya mkopo wa wanafunzi wa elimu ya juu. 
  3.  Uhakiki wa cheti cha kifo kwa ajili ya maombi ya mkopo wa wanafunzi wa elimu ya juu    
  4. Kubadili cheti cha zamani kupata cheti kipya

Vitu muhimu vya kuzingatia ni viwili au zaidi

  • Kadi Ya cliniki ya mwombaji
  • Prems number ya elimu ya sekondari
  • Prems namba ya elimu ya msingi
  • Kadi ya mpiga kura ya mwombaji
  • Tangazo la kizazi la mwombaji
  • Utambulisho wa wazazi (kitambulisho cha mpiga kura au utaifa wa wazazi)